Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga amewaagiza Viongozi mbalimbali katika Mkoa kutoa tahadhari kwa Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umegundulika huko Nchi jirani ya Kongo DRC.
Tahadhari hiyo imetolewa katika Kikao cha dharula cha Kamati ya Afya ya Mkoa amabayo imekutana kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola.
Kufuatia Shirika la Afya Dunia tarehe 08/05/2018 kutangaza kuwepo kwa Ugonjwa Hatari wa Ebola katika Nchi jirani ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo wagonjwa 21 wamegundulika na tayari 17 kati yao wameshapoteza maisha.
Kama mnavyofaha Mkoa wa Kigoma umepakana na Nchi jirani ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako Ugonjwa huu umegundulika.
Maeneo mbalimba ya muingiliano wananchi wametakiwa kuwa waangalifu, pamoja na vyombo vya usafiri, mipakani. Hivyo kutokana na muingiliano uliopo kati ya raia wa nchi zetu mbili ni vema tukaweka tahadhari kubwa kuzuia ugonjwa huo hatari usiingie nchini kwetu aliongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Wakiwasilisha taarifa za Ugonjwa huo, wataalam wa afya Mkoani Kigoma wamesema ugonjwa wa Ebola unaambukizwa kwa njia ya kugusa damu, au majimaji kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo,kugusa maiti ya mfu aliyekufa kwa Ebola, kugusa wanyama (mizoga na wanyama wazima) walioambukizwa kama vile Sokwe, Swala wa msituni.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa