Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango Asubuhi ya Leo Juni 23, 2023 amewasili mkoani Kigoma na kupokelewa na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye kisha kuelekea Mjini Kasulu amapo ameshiriki Ibada ya kumuombea Marehemu Midlaster Daniel Nsanzugwanko iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Mjini hapo.
Kupitia Salamu zake za pole, Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema kila mtu anapaswa kumheshimu Mungu na kuutambua utukufu wake bila kujali cheo, kazi au Mali alizonazo.
‘’Nilimfahamu Marehemu alipokuwa anasoma Chuo Kikuu Dar es Salaam, ambapo alikuwa ni mtu anayefahamu na kutekeleza vizuri kutekeleza wajibu wake wa kitaaluma’’ alisema Dkt. Mpango.
Makamu wa Rais amewaasa waombolezaji waliojitokeza na jamii kwa ujumla kujenga tabia ya kuweka pembeni tofauti zao za vyeo, siasa, dini na hata zile za kimitazamo na kuungana pamoja kwa ajili ya kuyakabili matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika Jamiii ikiwemo misiba.
Marehemu Midlaster alikuwa Mke wa Daniel Nzanzugwanko aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo Kasulu Mjini.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. PHILIP MPANGO AKITOA NENO LA FARAJA KWA WAFIWA PAMOJA NA WAOMBOLEZAJI (HAWAPO PICHANI) WALIOJITOKEZA KUSHIRIKI IBADA YA KUMUAGA MAREHEMU MIDLASTER DANIEL NSANZUGWANKOILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA LILILOPO MJINI KASULU.
DKT. PHILIP MPANGO AKISHUKA KWENYE NDEGE MARA BAADA KUWASILI UWANJA WA NDENGE WA MKOA WA KIGOMA.
DKT. PHILIP MPANGO AKISALIMIANA NA MWENYEJI WAKE KAMISHNA MSTAAFU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MHE. THOBIAS ANDENGENYE MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI KIGOMA.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA MHE THOBIAS ANDENGENYE AKITOA SALAMU ZAKE ZA POLE KWA FANILIA YA DANIEL NSANZUGWANKO NA WAOMBOLEZAJI WENGINE(HAWAPO PICHANI)
MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKIAGA MWILI WA MAREHEMU MIDLASTER DANIEL NSANZUGWANKO MARA BAADA YA IBADA YA MAOMBEZI KWA MAREHEMU ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA LILILOPO KASULU MJINI.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa