Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu umeazimia na kutoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM katika wilaya hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa kupitia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kasulu ulioketi Machi 24, 2025 kwa lengo la kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 kwa wilaya ya Kasulu katika kipindi cha hadi kufikia Februari 2025.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu Mbelwa Abdallah amesema chama kimefikia kutoa azimio hilo kufuatia kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi pamoja na utoaji wa huduma kwa wananchi wa Kasul, inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia.
Kupitia kikao hicho, Mbelwa amesema chama kitaendelea kuthamini na kutambua michango ya watendaji wa serikali katika wilaya hiyo watakaofanya vizuri katika kusimamia utoaji huduma bora kwa wananchi pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
Amesema chama kimekuwa kikikagua na kuridhishwa na hali ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika halmashauri ya wilaya na mji Kasulu, huku akiwapongeza wasimamizi wa miradi hiyo na kuwataka kutumia pongezi hizo kama chachu ya kufanya vizuri zaidi.
Katika hatua nyingine Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Kasulu imeipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 kwa wilaya hiyo hadi kufikia Februari 2025, iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa