Shirika la CARITAS KIGOMA limefanikiwa kuwajengea uwezo wakulima 1306 kuhusu Kanuni Bora za Kilimo katika Halmashauri za Kakonko, Kibondo, Uvinza, Buhigwe na Halmashauri ya Mji na Wilaya Kasulu katika kipindi cha Mwaka 2021/2022 hadi 2023.
Wakulima hao wamefanikiwa kujengewa uwezo katika matumizi sahihi ya Pembejeo, uelewa wa Kanuni Bora za Kilimo, Maarifa ya Kilimo cha Bustani pamoja na ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyeji walioboreshwa.
Akitoa Taarifa ya Utekelezeji wa Shirika la CARITAS-KIGOMA kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa, Katibu Tawala Mkoa Albert Msovela amesema Shirika hilo lisilo la kiserikali lilitoa vifaranga 6,000 vya kuku kwa makundi 39 ya wanufaika.
Aidha kupitia ujuzi walioupata wakulima hao wamefanikiwa kuvuna kuanzia Gunia 20 hadi 28 kwa Ekari zikiwa na ujazo wa Kilo mia moja kwa kila Gunia.
Msovela amezitaja Shughuli zilizofanywa na Shirika hilo la kidini mkoani Kigoma katika kipindi tajwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa Kilimo na Ufugaji, Ulinzi wa Mama na Mtoto kwa lengo la kupunguza Ukatili wa kijinsia katika Jamii.
Aidha shughuli nyingine zinazotekelezwa na Shirika hilo ni kuyajengea uwezo mabaraza ya Kata pamoja na kusaidia Jamii zinapotokea Dharura na Majanga.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa