Mkuu wa Mkoa wa Kigoma CGF(Mst) Thobias Andengenye( aliyekaa katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Wajumbe wapya wa Bodi ya Parole Mkoa wa Kigoma mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo.
Wakuu wa Magereza yaliyopo mkoani Kigoma wakiwa katika Picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, mara baada ya uzinduzi wa Bodi ya Parole ya Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika Viunga vya Bangwe Beach leo Tarehe 29 Agosti 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mhe. Thobias Andengenye amewataka Wajumbe wa Bodi ya PAROLE mkoani hapa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na Taratibu zinazoingoza bodi hiyo ili kutenda haki kwa wafungwa wanaostahili kunufaika na msamaha ili kumalizia adhabu zao nje ya Magereza.
Kauli hiyo ya Mkuu huyo wa Mkoa imetolewa wakati wa Hafla fupi ya Uzinduzi wa Bodi Mpya ya Parole mkoani Kigoma iliyofanyika katika viunga vya Bangwe Beach mjini hapa.
Andengenye amewataka wajumbe hao wapya kuepuka rushwa na upendeleo ili kubaini na kutoa haki kwa wafungwa wanaostahili, jambo ambalo litawaheshimisha na kuifanya Jamii iuthamini utumishi wao na kuwapa ushirikiano.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesisitiza matumizi sahihi ya Rasilimali chache zilizopo ili wajumbe hao waweze kuifikia jamii na kutoa Elimu kuhusu kazi za bodi hiyo hali itakayoongeza uelewa kwa wananchi kuhusu majukumu wanayoyatekeleza.
Kupitia risala kwa MgeniRasmi, ilibainishwa kuwa muitikio wa wananchi katika kushirikiana na bodi iliyipita ulikuwa ni hafifu kutokana na uwepo wa changamoto ya mawasiliano ambapo wajumbe wa bodi walishindwa kuifikia jamii kwa lengo la kutoa Elimu.
Aidha imeelezwa kuwa iwapo kazi za bodi hiyo zitafanyika kwa ukamilifu, zitapunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kutoa fursa kwa wenye sifa ya kupatiwa msamaha na bodi hiyo kumalizia sehemu ya vifungo vyao wakiwa nje ya Magereza huku wakiendeleza majukumu yao ya kijamii uraiani.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa