Taasisi za kifedha, mashirika na watu binafsi wameombwa kuendelea na moyo wa uzalendo wa kusaidiana na Serikali katika jitihada za kuimarisha huduma bora za afya na maendeleo katika sekta mbambali Mkoani Kigoma.
Haya yamelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mrindoka wakati akipokea vitanda 40 na magodoro yake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma vilivyotolewa na Benki ya Exim tawi la Kigoma kwa hospitali ya Rufaa ya Maweni.
Mhe. Mrindoko amesema anaishukuru Benki ya Exim kwa kwa kujali afya za wateja wao, “najua mnatambua kuwa ili wateja wenu waendelee kuzalisha lazima wawe na afya njema, na nyinyi mmelona hili hadi mmechangia kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali yetu, naombeni hata mashirika mengi pamoja na watu binafsi tuendelee kushirikiana na Serikali katika kuboresha sekta mbalimbali Mkoani Kigoma”. Aliongeza Mhe. Mlindoko.
Awali, akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya, Kaimu Mganga wa Mkoa Dkt. Kiza Kiseka alisema kuwa Hospitali ya Maweni inapaswa kuwa na vitanda 300, hata hivyo ilikuwa na upungufu wa vitanda 132 ambapo baada ya Benki ya Exim kutoa vitanda na magodoro 40 sasa upungufu umeshuka na kufikia 92. Vitanda vilivyotolewa na Benki ya Exim vitasaidia kupunguza adha ya wagonjwa kulala wawili katika kitanda kimoja.
Naye Meneja wa Benki ya Exim tawi la Kigoma Bw. Deo Makwaya amesema taasisi katika kuadhimisha miaka 20 ya kuwa kujali jamii ilipanga kuiunga mkoano sekta ya Afya kwa kutoa vitanda 500 kwa Mwaka huu katika hospitali 12 hapa Tanzania ambapo vitanda hivyo vimekuwa vikitolewa kila Mwezi.
Benki ya Exim pamoja na kujiwekea malengo haya ya mwaka mmoja kugawa vitanda 500, bado tutaendelea kujipanga kutoa na kuchangia si vitanda tu bali hata mahitaji mengine katika sekta ya afya, kwani tunaelewa bado hospili zetu zinahitaji mambo mbalimbali ya kuboresha afya.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa