Katika kuunga mkono uamuzi wa Serikali kulifanya zao la Tumbaku kuwa la Kimkakati, Benki ya CRDB Tawi la Kigoma, imekabidhi Pikipiki mbili aina ya Sanlg zenye Thamani ya Shilingi Mil 5.6 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ili ziweze kutatua changamoto ya usafiri kwa maafisa Ushirika katika wilaya za Uvinza na Kasulu Vijijini.
Akitoa neno la Shukurani mara baada ya kupokea pikipiki hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye, amesema pikipiki hizo zitawarahisishia maafisa Ushirika zoezi la kuwafikia wakulima wa tumbaku na kuleta matokeo chanya huku akisisitiza matumizi ya pikipiki hizo, yaendane na malengo yaliyowekwa.
‘’Pikipiki hizi ni mali ya wananchi na zikawanufaishe wao na sio maafisa ugani, hatutarajii pikipiki hizi zikasafirishe abiria au mizigo kwa maslahi ya mtu binafsi, bali zikalete matokeo chanya katika kilimo cha Tumbaku kwa maeneo zitakapotakiwa kutumika’’ amesema Andengenye.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kigoma Alison Andrew, amesema lengo la Benki yao kutoa Pikipiki hizo ni kuhakikisha wataalam wa Kilimo, wanawafikia wakulima wa zao la Tumbaku kwa urahisi ili kuongeza ufanisi na tija katika kilimo cha zao hilo mkoani hapa.
Amesema wakulima ni wadau muhimu wa Benki ya CRDB, hivyo kutolewa kwa Pikipiki hizo ni sehemu ya kuwagusa na kuwaunga mkono katika shughuli hiyo muhimu ya uzalishaji mali kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
‘‘Tunawatazama wakulima kama ni sehemu ya mafanikio yetu kwani ni wateja wetu wakubwa na tumeendelea kuwagusa kwa kuwapa mikopo kupitia AMCOS, kudhamini mafuzo mbalimbali pamoja na kuwawezesha vitendea kazi’’ amesema Alison.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa