• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

AWESO AKUTANA NA WADAU WA MAJI MANISPAA YA KIGOMA UJIJI

Posted on: July 16th, 2023


WAZIRI WA MAJI MHE. JUMA AWESO (KATIKATI) AKIWA KATIKA KIKAO CHA WADAU WA MAJI MANISPAA YA KIGOMA  UJIJI. KULIA KWAKE NI MKUU WA  MKOA  WA  KIGOMA  MHE. THOBIAS ANDENGENYE NA KUSHOTO NI KATIBU TAWALA  MKOA  WA  KIGOMA  MHE. ALBERT MSOVELA.

Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso (Mb) amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha na kuimarisha Miundombinu ya Maji nchini ili kuwaondolea wananchi adha zitokanazo na changamoto ya ukosefu wa huduma hiyo.

Waziri Aweso amesema hayo alipozungumza kwenye kikao cha pamoja kilichomkutanisha na wadau wa Maji katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Hapa.

Waziri Aweso amesema pamoja na kuendelea kuimarika kwa upatikanaji wa Huduma hiyo Mkoani Kigoma, Serikali itaendelea kuhakikisha Maji yanayopatikana ni Safi, toshelevu na yenye ubora unaostahili kwa matumizi ya binadamu.

Amefafanua kuwa, Serikali inaendelea na Mchakato wa kuhakikisha Ziwa Tanganyika linakuwa chanzo kikuu na cha uhakika cha uzalishaji wa Maji yatakayotumiwa na wakazi katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi.

Aweso ametoa wito kwa wadau wa Maendeleo wanaotaka kuwekeza mjini Kigoma kutekeleza adhma hiyo ya kimaendeleo kutokana na utoshelevu wa Maji ambapo kwa sasa uzalishaji umefikia kiasi cha  Lita Mil. 42 huku mahitaji halisi yakiwa ni lita Mil. 23.

Pia Waziri ameielekeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji kutokuwa kikwazo katika zoezi la usambazaji na utoaji wa huduma nyinginezo zinazohusu Maji kwa lengo la kusogeza na kuongeza hali ya utoaji wa huduma hiyo  kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa KigomaThobias Andengenye amesema Jumla ya Vijiji 306 vimepatiwa huduma ya Maji huku vingine 40 vikiwa havijafikiwa kabisa huku upatikanaji wa huduma hiyo ukipanda kutoka Asilimia 56 hadi kufikia Asilimia 67.3.

‘’Katika kukabiliana na changamoto hiyo Serikali inaendelea kutekeleza ujenzi wa miradi ya Maji 49 katika vijiji 77 ambayo inatarajia kukamilika 2025 na kusababisha ongezeko la Asilimia 17.8 ya upatiakaji wa Maji mkoani hapa’’ amesema.

Ameendelea kusema kuwa, kazi mbalimbali zimeendelea kufanyika ikiwemo kutoa Elimu na kuhamasisha utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji kwa kuhamasisha upandaji wa miti rafiki kwa Mazingira.

Upande wake Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kigoma Ujiji Poas Kilangi, amemueleza Waziri kuwa, katika Manispaa ya Kigoma Ujiji yenye kata 19 ikiwa na wateja hai wa Huduma hiyo 17, 347, mtandao wa Maji umefikia Km. 405.

Amezitaja chanagamoto zinazowakabili kiutendaji ikiwemo uchakavu wa Jengo la Ofisi, uhaba wa watumishi pamoja na kutotosheleza kwa vitendea kazi ikiwemo uhaba wa vyombo vya Usafiri.

Pia ameutaja udogo na uchakavu wa mabomba kuchangia kwa kiasi kikubwa kutopatikana  kwa huduma ya uhakika ya  maji katika baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Aidha katika kudhibiti matumizi ya holela ya Maji, Kilangi amesema wamefanikiwa kuagiza mita za Maji 2500 na wanaendelea kuzifunga kwa wateja ili kila mtu achangie  huduma hiyo kuendana na matumizi yake.

Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • RC ANDENGENYE AKABIDHI VITENGO VITENGO VYA LISHE MKOA NA WILAYA UVINZA

    May 09, 2025
  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa