NA GRADNESS KUSAGA-KIGOMA.
Serikali Mkoani Kigoma kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii imefanikiwa kuwapatia Jumla ya wazee 42,202 sawa na Asilimia 77 vitambulisho vya matibabu huku wazee 3100 wakiunganishwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) kwa lengo la kuwapunguzia usumbufu wakati wa matibabu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo kimkoa imefanyika katika Ukumbi wa Joy in The Harvest Manispaa ya Kigima/Ujiji
Amesema kuwa hadi sasa Hospitali 8 za Halmashauri za mkoa zimefanikiwa kuanzisha madirisha ya matibabu kwa wazee kwa lengo la kupunguza adha ya kusubiri upatikanaji wa matibabu kwa muda mrefu.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema Mkoa wa Kigoma umeendelea kuunda mabaraza ya wazee katika ngazi zote kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee hao ili kupata ufumbuzi wa pamoja na kuimarisha upatikanaji wa haki na Huduma sahihi‘’ amesema Kalli.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Lebba akimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa kigoma, amesema wazee ni hazina na tunu hivyo jamii iendelee kuwatunza kwa kuwapatia kipaumbele katika mambo yote ili kuendelea kunufaika na ushauri pamoja na Maelekezo yao.
‘’Serikali mkoani Kigoma itaendelea kuhakikisha inatoa usaidizi kwa wazee ili waweze kuishi katika Mazingira Salama na endelevu ambayo yatawapunguzia changamoto zitokanazo na mabadiliko yanayosababishwa na kukua kwa Teknolojia pamoja na Maendeleo kwa ujumla’’ Amesema Lebba.
Naye katibu wa Baraza la wazee Mkoa Gideon Menyo ameishukuru Serikali kwa kufanya utafiti katika Hospitali binafsi pamoja na mashirika mbalimbali yanayotoa huduma za Jamii ili kuhakikisha wazee wanapewa kipaumbele katika upatikanaji wa huduma mbalimbali na kwa wakati.
‘’Tunafurahishwa na Huduma ya Mpishe Mzee kwanza’’ ambayo kupunguza athari ambazo zingejitokeza kwa wazee kutokana na kukosa huduma ikiwemo zile za matibabu kwa muda muafaka’’ Mzee Menyo
Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani yamehudhuriwa na Katibu Tawala mkoa, Makatibu Tawala wasidizi Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa, Wataalamu kutoka mamlaka za serikali za mitaa, Wakuu na wawakilishi wa taasisi za serikali na taasisi zisizo za kiserikali za Help Age Tanzania, REDESO, IRC na EWAK, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na madhehebu ya Dini.
Kauli mbiu ya Maadhimisho jayo kwa Mwaka 2023 yamebeba ujumbe usemao ‘’Uthabiti wa wazee kwenye Dunia Yenye Mabadiliko’’.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa