Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mst. Thobias Andengenye amesema zoezi la uwekaji wa Anwani za makazi litasaidia katika kupanga na kuwafikishia maendeleo kwa urahisi na wepesi wananchi katika maeneo yao.
Andengenye amesema haya wakati akizindua rasmi maandalizi ya Operesheni ya uhamasishaji wa uwekaji wa anuani za makazi Mkoa wa Kigoma na kuongeza kuwa itasaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya watu na pia kuokoa muda na rasilimali katika kufikisha huduma kwa wanachi kwa mfano kuagiza bidhaa sokoni na bidhaa hiyo kukufikia nyumbani kwako kwa haraka na usahihi.
Kama mtakumbuka nchi yetu mwaka 2019 iliingia kwenye uchumi wa kati. inamaanisha nchi imepiga hatua kimaendelea katika Nyanja mbalimbali, maendeleo ambayo yanapaswa yaakisi pia kwenye mipango yetu ya huduma kwa wananchi ili kuendana na ukuaji wa uchumi unaochagizwa na matumizi mazuri ya Teknolojia kama kuwa na anuani za makazi.
Kutokana na maendeleo ya kidijitali kila mtanzania atapaswa kujulikana kwa urahisi maeneo anakoishi na au anakofanyia kazi ni utambulisho wa mahali mtu/ kitu kilipo juu ya uso wa ardhi. Aina hii ya utambulisho inaundwa na namba ya anuani, jina la barabara au mtaa na postikodi. Zoezi hili linalenga kurahisisha utambuzi wa makazi ambao ndio ustarabu wa dunia kumtambulisha mtu anapoishi nahii ni hatua muhimu sana katika suala zima la kimaendeleo kwa dunia ya sasa.
Amewaagiza wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Mkoani Kigoma kuhakikisha kuwa zoezi linafanyika na kukamilika kikamilifu ndani ya muda uliopangwa. Zoezi la kubaini anwani na makazi linategemewa kuwa limekamilika ifikapo mwezi Mei, mwaka 2022.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa