Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema kukamilika kwa ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR, kutatoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kusafirisha bidhaa zao kwa muda mfupi na gharama nafuu hali itakayowaletea tija kiuchumi.
Andengenye ametoa kauli hiyo alipokutana na ujumbe kutoka Shirika la Reli Tanzania(TRC) kwa lengo la kupokea Taarifa ya Maandalizi ya uwekwaji wa Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) Km. 506 kutoka Tabora hadi Kigoma.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa, mradi huo utaongeza fursa za Ajira pamoja na kupanua mzunguuko wa biashara mkoani hapa.
Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Albert Msovela amesisitiza kuwa utolewaji wa ajira zisizohitaji utaalam wakati wa utekelezaji wa Mradi huo utoe kipaumbele kwa wakazi wenyeji ili waweze kunufaika kiuchumi na kuziona faida za Mradi kutekelezwa katika maeneo yao.
Pia Msovela ametoa wito kwa wakazi mkoani Kigoma nan chi jirani kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazojitokeza wakati na baada ya ujenzi wa mradi huo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa