Leo Juni 7, 2023 RC Andengenye amefungua na kushiriki Mkutano wa Baraza la Madiwani Wilaya ya Kigoma Vijijini kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2022.
Kupitia hotuba aliyoitoa kwenye Mkutano huo, Andengenye amesisitiza uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato pamoja na kudhibiti upotevu wa Fedha za Makusanyo unaofanywa na baadhi ya watumishi wanaosimamia jukumu hilo wasio waaminifu.
Kadhalika, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Rose Manumba ameahidi kufanya maboresho makubwa katika zoezi zima la uibuaji na ufuatiliaji makusanyo ya ndani huku akisisitiza kuendelea kudumisha ushirikiano baina ya wataalam na wananchi ili kutatua changamoto mbalimbali katika utoaji wa Huduma za Kijamii katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye akizungumza na Wah. Madiwani (hawapo pichani) wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, kupokea na kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2022. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma vijijini uliopo katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Juni 7, 2023.
Mhe. Albert Msovela ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma akifuatilia Jambo katika Mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Rose Manumba akifuatilia jambo katika mkutano huo.
waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wakifuatilia Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2022 kupitia Makabrasha yao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa