Mkoa wa Kigoma sasa umekuwa ni kivutio kikubwa cha wawekezaji wa aina mbalimbali. Hii inatokana na ukweli kwamba ni njia fupi ya kibiashara inayounganisha Bandari ya Kigoma na Eneo lote la Maziwa Mkuu na Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi kupitia Reli ya Kati, Barabara ya Kati na Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Mkoa ni mlango wa Biashara za kimataifa na imekuwa ni mvuto wa wawekezaji, imedhihirika kuwa Kigoma ni eneo zuri kimkakati kuendeleza Eneo Maalum la Uchumi kutoa huduma kwa nchi zinazolizunguka Ziwa Tanganyika.
Mkoa unaendesha mradi wa kuendeleza Eneo Maalum la Kiuchumi (Kigoma Special Economic Zone “KiSEZ”). Eneo la hekta 20,000 limeainishwa lakini kutokana na uwezo wa kifedha, Mkoa umepanga kutekeleza kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza ina jumla ya hekta 691 na tayari shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwa ni pamoja na:-
Mpango wa kuendeleza Eneo Maalum la Kiuchumi Kigoma (KiSEZ) umefikia mahali ambapo ni muhimu kukamilisha malipo ya fidia na kuweka miundombinu ya nje, ili kuunga mkono juhudi za serikali ambazo zimekwishafanyika hadi sasa kuliendeleza eneo hilo.
Mkoa umeendelea kuchukua hatua za kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na hivyo kupata wawekezaji makini wanne hadi sasa. Wawekezaji wawili wamejikita kwenye kilimo ambapo mwekezaji wa kwanza ni Kampuni ya Agrisol (T) Ltd. Kampuni hiyo iwepewa eneo katika Wilaya ya Kigoma eneo la Lugufu, ambapo watalima Maharage na Mahindi. Kampuni hii imeshafuata taratibu zote za uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na wanaanza kazi kwa kusafisha eneo la awamu ya kwanza lenye 500Ha wiki ijayo. Eneo hili watalima Mahindi 250Ha na Maharage ya Soya 250Ha; vile vile kampuni itajihusisha na usindikaji wa mazao yanayozalishwa katika shamba hilo. Mradi huu unataraijiwa kunufaisha wananchi katika ajira na kilimo cha mikataba (Outgrowers Scheme).
Kampuni ya pili inayowekeza kwenye kilimo inaitwa Kigoma Sugars Ltd. Ambapo itashughulikia kilimo cha Miwa katika Wilaya ya Kasulu, ambapo watajenga kiwanda cha sukari na kufua umeme wa mabaki ya miwa. Kampuni hiyo iko katika hatua za kukamilisha taratibu za uwekezaji kwenye kituo cha uwekezaji (TIC). Mradi huo utatekelezwa kwenye eneo la hekta 47,000 na unatarajiwa kuwa ni mradi mkubwa kuliko yote nchini, utakuwa unazalisha tani 6,000 kwa siku. Hivyo, mradi huo utaleta manufaa kwa wananchi katika ajira na kilimo cha mikataba (Outgrowers Scheme).
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255738192977
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa