Fursa nyingine kwa wanakigoma na Mikoa Jirani ambapo Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na TCCIA (Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture), Tanzania Investment Centre (TIC), LIC (Local Investment Climate), TANTRADE, TNBC (Tanzania National Business Council), AGRA (Alliance for a Green Revolution in Africa) na Afro Premiere unaandaa kongamano la kwanza la Kimataifa la kibiashara Tanganyika Business Summit & Festival’ litakalofanyika kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 11 Mei 2019 katika ukumbi wa mikutano wa NSSF-Kigoma.
Kongamano linalengo la kukuza biashara na uwekezaji Mkoani Kigoma kwa kutumia fursa za nchi jirani za Burundi, DRC Congo, Zambia, na Rwanda.
Kongamano linatarajiwa kuwa na washiriki wapatao 300 na washiriki wa maonyesho (Exhibitors) 150 kutoka ndani na nje ya Nchi.
Hii ni fursa kubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma kutoa taswira ya kibiashara, uwekezaji na kuwavutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza Mkoani Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa