Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amekutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa na Dini kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Amesema Jumla ya Vijiji 306, vitongoji 1,858 na Mitaa 176 itahusika na uchaguzi huo huku uchaguzi ukilenga kupatikana kwa wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri za vijiji, wenyeviti wa vitongoji, wenyeviti wa Mitaa, wajumbe Kamati za Mitaa pamoja na wenyeviti wa vitongoji huku ukihusisha vituo 2252 vya kupigia kura.
Amewataka wawakilishi hao kwenda kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa lengo la kupiga kura au kupigiwa kura ili nchi iweze kupata viongozi bora watakaotokana na maamuzi ya wananchi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia Makini Mkoa wa Kigoma Ramadhani Kwezi amesema ameridhishwa na hatua za awali kuelekea uchaguzi huo ikiwemo ushirikishwaji wa vyama vya Siasa katika hatua zote za Maandalizi ya uchaguzi huo.
Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa(TCD) wilaya ya Kigoma Yassin Bakari amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuimarisha Demokrasia ikiwemo kutoa fursa sawa kwa vyama vya siasa katika kushiriki michakato ya uchaguzi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa