Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) wametakiwa kuimarisha mfumo wa kuwafikia wadau badala ya kusubiri kufuatwa na wadau hao katika maeneo yao ya kutolea huduma.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipozungumza wakati akifungua kikao cha wadau wa wakala huyo, kilichofanyika Mjini Kigoma.
Amesema umefika wakati TEMESA wanatakiwa kuanza kuwafuata wateja wao katika maeneo walipo na kuwapatia huduma, jambo litakaloongeza kasi ya kuzifikia na kuzihudumia Taasisi, Idara na Wakala wa Serikali.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wadau wote wanaohudumiwa na wakala huyo kulipia huduma wanazopatiwa kwa wakati ili Taasisi hiyo iweze kujiendesha kwa tija.
‘’wasimamizi wa vyombo vya usafiri hakikisheni vyombo hivyo vinapelekewa kwenye matengenezo kwa wakati kwani vinapocheleweshwa husababisha ongezeko kubwa la gharama za matengenezo’’ amesema Andengenye.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameutaka Uongozi wa TEMESA kutumia fursa ya maboresho makubwa yanayofanywa na Serikali kuimarisha utaratibu wa utoaji wa Huduma kwa wadau wao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa