Waratibu wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mkoani Kigoma wametakiwa kuwajengea uwezo wanufaika wa mradi huo ili waweze kufuzu na kumudu kujitegemea kiuchumi kwa lengo la kuachana na utegemezi wa mfuko huo katika kuendesha maisha yao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipozungumza wakati akifungua Kikao kazi cha Viongozi wa Mkoa na Wilaya kilichofanyika mjini Kasulu na kusisitiza kuwa wanufaika wanapaswa kutumia fedha wanazozipata kuibua miradi itakayowafanya waweze kujitegemea.
Amesema wanufaika wanapofikia hatua ya kufuzu na kuanza kujitegemea, wanatoa fursa kwa au kukosa nafasi katika mpango wa awali kutoa fursa kwa wahitaji wapya ili kuongeza idadi ya watanzania watakaoguswa na huduma za mfuko huo.
Ameeleza kuwa, sambamba na kuwajengea uwezo wanufaika, watendaji hao wanapaswa kupiga hatua zaidi kwa kuijengea uelewa jamii kwa ujumla wake kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa kutoa taarifa kuhusu hatua mbalimbali zinazofikiwa.
Amewasisitiza wajumbe wa kikao hicho kuhakikisha wanakuwa ni sehemu ya utekelezaji kwa sambamba na kutoka na majibu pale ambapo jamii itahitaji majibu kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji mradi sambamba na taratibu zinazoongoza katika kutoa maamuzi.
Kikao hiki kitatupatia dira mpya na kuwezesha kila mmoja wetu kuwa mwalimu na sehemu ya utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo wananchi kuhusu hatua mbalumbali za utekelezaji wa mradi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa