Watu nane wamefariki Dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia ajali ya Gari ndogo Aina ya Toyota Succeed yenye Namba T890 DYZ iliyokuwa ikisafirisha abiria katika Wilaya za Kibondo na Kakonko kugongana na gari aina ya Faw Namba T833 DUA mali ya Kampuni ya CHICO katika kijiji cha Kamkugwa wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataja waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea Desemba 23, 2023 ni Hamis dereva na mmiliki wa gari ndogo Hamisi Chaurembo(27) waliokuwa abiria Bernadina Reuben(22), Maduha Asukile, Ntinganiza Bihezako(67) Vedastus Paul(28), Vladmir Vedastus(1) na marehemu wawili ambao majina yao bado hayajafahamika.
Amewataja majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni Flavianus Felician(28), Juma Said(27), Daniel Samwel,(33) Silvanus Muhingwa(43), Sara Bundala(20), Doris Mafumbo(22), ambapo watatu kati yao wamepelekewa Hospitali ya Rufaa Bugando huku wengine wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya wilaya Kibondo.
Andengenye ametoa Rai kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri mkoani Kigoma kuendelea kuchukua tahadhari wawapo barabarani ikiwemo kuzingatia alama za usalama barabarani pamoja na kuepuka mwendo kasi.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameikumbusha jamii kuchukua tahadhari mbalimbali za kiusalama hususani kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa