Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig.Gen. (Mst.) Emmanuel Maganga amekutana na Mhe. Dan Kazungu Balozi wa Kenya nchini Tanzania na kufanya mazungumzo juu ya kuwaunganisha Watanzania na Wakenya katika kutumia fursa za kibiashara zilizomo Mkoani Kigoma.
Maganga amemwambia Balozi wa Kenya kuwa Mkoa wa Kigoma ni lango kuu la nchi jirani za Burundi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda na Zambia.
Amemuhakikishia kuwa Kigoma inafursa nyingi ambazo kwa hakika wawekezaji wakiwa na nia ya kuja kuwekeza Mkoani Kigoma wanakaribishwa.
Kwa upande wake Mhe. Kazungu amesema ameamua kutoka ofisini ili kuja kujionea mwenyewe mambo mazuri ambayo ni vivutio kwa uwekezaji katika Mkoa wa Kigoma ambapo amesema "nimefurahi kufika katika mji huu wa kihistoria ambao unavivutio vingi vya kuweza kwenda kuwashawishi wakenya kuja kuwekeza Mkoani Kigoma"
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa